Thursday, November 17, 2011

If you yelled for 8 years, 7 months and 6 days, you would have produced enough sound energy to heat one cup of coffee.
Chewing gum while peeling onions will keep you from crying!

Wednesday, November 16, 2011

Did You Know???








  • Did you know that there are 206 bones in the adult human body and there are 300 in children (as they grow some of the bones fuse together).
  • The most dangerous animal in the world is the common housefly. Because of their habits of visiting animal waste, they transmit more diseases than any other animal.
  • Koalas and humans have similar, unique fingerprints.
  • The longest cells in the human body are the motor neurons. They can be up to 4.5 feet (1.37 meters) long and run from the lower spinal cord to the big toe.
  • The human eye blinks an average of 4,200,000 times a year.
  • The longest living cells in the body are brain cells which can live an entire lifetime.
  • Borazon is one of the hardest substances in the world, which is a combination of Boron and nitrogen. it is so hard, it can even scratch a real diamond.
  • Every year about 98% of the atoms in your body are replaced.
  • When you combine a question mark (?) with an exclamation point (!), it’s called an “interrobang”.

Tuesday, November 15, 2011

Serikali Iombe Wananchi Msamaha - Mgao wa Umeme

Imeripotiwa kuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ameitaka serikali iwaombe radhi wananchi kwa mgao wa umeme unaoendelea. Kauli hiyo ya Sitta imewafanya maadui wake ndani ya serikali, CCM na baadhi ya vyombo vya habari vinavyotumiwa kuibuka na kumuita waziri huyo kuwa ni msaliti na lazima afukuzwe kazi.Lazima tukubali kuwa tuna tatizo kubwa sana la uwajibikaji katika nchi hii. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata umeme kwa ajili ya kuhakikisha ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa huduma za jamii na maisha ya kila siku ya wananchi.


Leo hii, wastani wa asilimia 15 tu ya Watanzania milioni 44 wanapata umeme.Na serikali imeshindwa kuhakikisha kuwa asilimia hiyo ndogo ya wanaopata umeme wanapata huduma ya uhakika. Hapa ndipo dhana ya uwajibikaji inapokuja.

Kitendo cha serikali yenyewe kulazimika kuitoa bajeti ya wizara ya nishati na madini Bungeni ili
wakajipange upya ni ishara nyingine kuwa serikali haiko makini kwenye kutatua mgao wa umeme. Ni baada tu ya kuona kuwa Wabunge wamekuja juu na huenda hawatapitisha bajeti hiyo ndiyo serikali ikashituka usingizini na kusema wanahitaji muda wa kujipanga zaidi.

Wakati serikali imeongeza bajeti ya miundombinu kwa asilimia 85 na kufikia shilingi trilioni 2.78 ($1.73 billion), ilitenga shilingi bilioni 402.4 ($250m) tu kwa wizara ya nishati na madini katika kipindi hiki ambacho taifa liko kwenye janga kubwa la umeme. Ni kweli tunahitaji barabara, bandari, reli na airport, lakini ni lazima tuweke vipaumbele sawa. Kama pesa hazitoshi kufanya vyote kwa wakati mmoja, serikali makini ingetatua tatizo la umeme kwanza ndipo ijenge barabara.

Narudia tena, tatizo la umeme nchini si ukame. Ni matokeo ya serikali kutotoa kipaumbele kwa suala hili tangu ilipoingia madarakani. Ndiyo maana serikali imekiri yenyewe kuwa katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano, imeongeza megawati 145 tu kwenye gridi ya taifa. Lazima kuwe na hatua za dharura, muda mfupi na muda mrefu (immediate, medium-term na long-term) za kukabiliana na tatizo hili. Serikali inabidi isimamishe safari za nje, posho, semina, manunuzi ya Landruiser VX, na matumizi mengine ya anasa ili pesa zote ziende kwenye umeme. Na ikibidi hata ikope pesa nje ili kuwekeza kwenye umeme. Kwenye global financial crisis, serikali ilitoa 1.7 trillion shillings (over $1 billion) na kugawa pesa hizi kwa kampuni zenye utata. Leo hii serikali inasemaje haina pesa za kuzalisha umeme na kutoa $250m tu? Athari za mgao wa umeme ni kubwa mara dufu kuliko zile za global financial crisis.

Serikali inabidi ifanye budget re-allocation kubwa na kutoa pesa kwenye wizara na mufungu mengine na kuzipeleka kwenye umeme.

Huko Afrika Kusini mwaka 2008 wakati nchi hiyo ilipokutwa na tatizo la umeme, aliyekuwa Rais wa wakati huo, Thabo Mbeki, alikuwa na uungwana wa kwenda mbele ya Bunge la nchi hiyo na kuwaomba radhi wananchi kwa mgao wa umeme. Sijaona mkuu wa nchi yetu akichukua hatua kama hii.

Thabo Mbeki alisema kuwa Eskom (TANESCO ya Afrika Kusini) ilikuwa inaomba pesa serikalini kila siku iwekeze kwenye umeme serikali ikakataa na kuwambia wasubiri mpaka baadae. Mbeki akakiri kuwa Eskom ilikuwa sahihi na serikali ilikosea. Na akaomba radhi. Wataalamu wa TANESCO waliikataa Richmond, vigogo serikalini wakalazimisha wapewe mkataba na matokeo yake tumeyaona. Hakuna aliyeomba radhi, na mhusika kuu akabaki kusema hajutii maamuzi yake na kujisifu kuwa yeye ni hodari wa kufanya maamuzi magumu. TANESCO kila siku imekuwa ikiomba pesa za miradi mikubwa ya umeme lakini serikali imekuwa ikiwaambia waendelee kusubiri tu. Hakuna aliyekiri kosa, kuomba radhi wala
kuwajibika.

Angalia:
http://www.news24.com/SouthAfrica/Politics/Mbeki-apologises-for-power-cuts-20080208-2
http://www.iol.co.za/news/politics/mbeki-apologises-for-sa-power-cuts-1.382421
http://www.southafrica.info/about/government/stateofnation2008-electricity.htm

Idara ya hali ya hewa iko pale kufanya utabiri wa hali ya hewa. Hivyo basi, tangu mwaka 2005 walitabiri kuwa 2010/11 kutakuwa na upungufu wa mvua. Hata hii leo wanaweza kutoa utabiri wa hali ya hewa ya mwaka 2015/16 itakuwaje. Serikali ilikuwa na taarifa tangu miaka mitano au hata kumi iliyopita kuwa mwaka huu kutakuwa na mvua chache na hii itaathiri uzalishaji wa umeme, upatikanaji wa chakula, mfumuko wa bei, nk. Serikali iache kusingizia ukame. Iombe radhi kwa taifa kuwa mgao huu wa umeme unatokana na serikali yenyewe kutotoa kipaumbele kwa tatizo hili na kutojipanga kukabiliana nalo. Na iseme ukweli chanzo cha mgao ni nini, umeleta athari gani kwa taifa, serikali inafanya nini na tatizo hili litaisha lini. Serikali sikivu ingewaomba radhi wananchi wake. Na wananchi makini na wazalendo wangedai uwajibikaji kutoka serikalini, si visingizio vya ukame!




fromhttp://swahilitime.blogspot.com/2011/07/serikali-iombe-wananchi-msamaha-mgao-wa.html

Boat floating on Air......is this real..


this toy boat is seen to float on an invinible fluid

Monday, November 14, 2011

Waturuki wai 'HACK' website ya microsoft

Kundi hilo linalojulikana kama “Terrorist crew” liliiteka kwa masaa kadhaa website ya Microsoft maalumu kwa nchi ya Ireland na kuwaachia wadau wa website hiyo salamu za idi Mubarak.

Mwaka 2006 kundi jingine la waturuki liliiteka website ya Microsoft ya Ufaransa na kuwaachia wadau wa Microsoft ujumbe huu:
"Hi Master (: Your System 0wned By Turkish Hackers! redLine ownz y0u! Special Thanx And Gretz RudeBoy |SacRedSeer| The_Bekir And All Turkish HacKers next target: microsoft.com date: 18/06/2006 @ 19:06 WE WERE HERE...."

Kundi la vijana wa kituruki limekuwa likishindana na kundi la vijana wengine wa Urusi katika kuziteka tovuti mbali mbali duniani.

Mwaka 2005 kundi hilo lilifanikiwa kuziteka computer za vyombo vikubwa vya habari vya marekani kama vile CNN, New York Times, ABD News na vinginevyo na kufanikiwa kutuma virusi kibao ambavyo vilivuruga mitambo yao.

Mojawapo ya tovuti zilizowahi kutekwa na kundi la waturuki ni tovuti ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uraisi wa Marekani kupitia chama cha Republican Duncan Hunter,tovuti ya chama cha soka cha Denmark ,tovuti ya NGO moja ya kupambana na ukimwi nchini Ufaransa ya Solydays.

Katika tukio la jana vijana hao waliwashangaza wadau wa Microsoft waliotembelea tovuti hiyo jumanne asubuhi kwa kukuta meseji ya EID MUBARAK na meseji yao ya kujipongeza kwa kuiteka website hiyo.

Hata hivyo wataalamu wa microsoft walifanikiwa kurekebisha tatizo hilo ingawa liliwachukua masaa kadhaa.

Msemaji wa Microsoft Ireland alisema "Hakukuwa na ubadhirifu wowote uliofanyika kutokana na tukio hilo".

"Kulikuwa na mapungufu katika ulinzi wa tovuti yatu ,Wataalamu wetu wanashughulikia tatizo hili ili lisitokee tena " aliongeza msemaji huyo.

Tanzania 2010/2011 Government Budget

to view the budget click on the link below

Link:Tanzania 2010/2011 budget

Blogroll